Nafasi za kazi Halmashauri ya Wilaya ya Songwe December 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba ajira katika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe baada ya kupokea kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:
DEREVA DARAJA II
Halmashauri ya Wilaya ya Songwe
5 Positions
Application Period
24/12/2025 – 06/01/2026
Duties and Responsibilities
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
- Kufanya usafi wa gari; na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
Qualifications
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Remuneration
TGS B