Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo anawatangazia Watanzania wote wenye sifa kuomba ajira katika Halmashauri hii kwa nafasi saba (7), baada ya kupokea kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kama ifuatavyo:
1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 02
1.1 MAJUKUMU NA KAZI
Mwajiriwa atatekeleza majukumu yafuatayo:
i. Kuorodhesha barua zinazoingia Masijala katika Rejista ya barua zinazoingia (Incoming Correspondence Register);
ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi katika Rejista ya barua zinazotoka (Outgoing Correspondence Register);
iii. Kusambaza majalada kwa Watendaji (Action Officers);
iv. Kupokea majalada yanayorejeshwa Masijala kutoka kwa Watendaji;
v. Kutafuta kumbukumbu, nyaraka na majalada yanayohitajika na Watendaji;
vi. Kurudisha majalada katika kabati au maeneo rasmi ya kuhifadhia (Filing Cabinets/Racks);
vii. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (File Tracking);
viii. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa kuwa:
-
Mhitu wa Kidato cha Nne au Kidato cha Sita (Form IV au VI);
-
Mwenye Stashahada (Diploma) au Cheti cha NTA Level 6 ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali;
-
Mwenye ujuzi wa matumizi ya Kompyuta.
1.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS C
2.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 05
2.1 MAJUKUMU NA KAZI
Mwajiriwa atatekeleza majukumu yafuatayo:
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama;
ii. Kuwapeleka Watumishi katika safari mbalimbali za kikazi;
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika Daftari la Safari (Log Book);
vi. Kufanya usafi wa gari;
vii. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa kuwa:
-
Mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV);
-
Mwenye Leseni halali ya Udereva Daraja E au C;
-
Awe na uzoefu wa kuendesha gari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali;
-
Awe na vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyompa sifa ya kupata madaraja husika;
-
Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Udereva (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
2.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS B
3.0 MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45;
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na wanapaswa kubainisha hali zao kwenye mfumo wa maombi ya ajira;
iii. Waombaji waambatishe Cheti cha Kuzaliwa kilichothibitishwa kisheria;
iv. Waombaji waambatishe Wasifu Binafsi (Detailed CV) wenye anuani, namba za simu zinazopatikana na majina ya wadhamini watatu (3);
v. Waombaji waambatishe nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili;
vi. Testimonials, Provisional Results, Statements of Results na Result Slips za Kidato cha Nne na Sita HAVITAKUBALIWA;
vii. Waombaji wawe na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA);
viii. Waombaji wenye tofauti za majina waambatishe Hati ya Kubadili Jina (Deed Poll);
ix. Waombaji wenye tofauti za herufi waambatishe Kiapo (Affidavit);
x. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na NECTA, TCU au NACTE;
xi. Waombaji wawe hawajawahi kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai;
xii. Waombaji waliopo katika Utumishi wa Umma kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba;
xiii. Waombaji watakaobainika kutoa taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria;
xiv. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 17 Januari, 2026.
MUHIMU
Waombaji wanapaswa kuambatisha Barua ya Maombi ya Kazi iliyosainiwa, ikielekezwa kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA GAIRO
S.L.P 40,
GAIRO
NJIA YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kwa anuani ifuatayo:
👉 https://portal.ajira.go.tz
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliobainishwa HAYATAFIKIRIWA.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA GAIRO