Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati anawatangazia Watanzania wote wenye sifa kuomba ajira katika Halmashauri hii kwa nafasi kumi (10), baada ya kupokea kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kama ifuatavyo:
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 06
1.1 MAJUKUMU NA KAZI
Mwajiriwa atatekeleza majukumu yafuatayo:
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
ii. Kupokea wageni, kuwasikiliza na kuwaelekeza sehemu husika kwa ajili ya kushughulikiwa.
iii. Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake pamoja na ratiba za kazi.
iv. Kutafuta na kuandaa majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
v. Kupokea na kusambaza majalada kwa Maafisa katika Idara/Vitengo husika.
vi. Kukusanya, kutunza na kurejesha majalada na nyaraka sehemu stahiki.
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa kuwa na:
-
Elimu ya Kidato cha Nne au Sita;
-
Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili;
-
Uwezo wa kuandika kwa hatimkato (shorthand) kwa Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika;
-
Ujuzi wa matumizi ya programu za Kompyuta za Ofisi kama vile Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS C
2.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 04
2.1 MAJUKUMU NA KAZI
Mwajiriwa atatekeleza majukumu yafuatayo:
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari kwa ajili ya usalama.
ii. Kuwapeleka watumishi katika safari mbalimbali za kikazi.
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
iv. Kutunza na kuandika daftari la safari (Log Book).
v. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
vi. Kufanya usafi wa gari.
vii. Kufanya kazi nyingine atakazoelekezwa na Msimamizi wake.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa kuwa na:
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV);
-
Leseni halali ya Udereva Daraja E au C;
-
Uzoefu wa kuendesha magari kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali;
-
Vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyompa sifa ya kupata daraja husika;
-
Cheti cha mafunzo ya msingi ya Udereva (Basic Driving Course) kutoka Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
2.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS B
3.0 MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na wanapaswa kuainisha ulemavu wao katika mfumo wa maombi ya ajira.
iii. Waombaji waambatishe Wasifu Binafsi (Detailed CV) unaojitosheleza, ukiwa na anuani, namba za simu, barua pepe pamoja na majina ya wadhamini watatu (3) wa kuaminika.
iv. Waombaji waambatishe nakala za vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa kisheria.
v. Testimonials, Provisional Results, Statements of Results na Result Slips HAVITAKUBALIWA.
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA au NACTVET).
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wawe na kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
viii. Waombaji wa Kada ya Dereva waambatishe vyeti halali vya mafunzo ya Udereva.
ix. Waombaji waliopo katika Utumishi wa Umma kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
x. Waombaji watakaobainika kutoa taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Waombaji wenye tofauti za majina katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll).
xii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 16 Januari, 2026.
xiii. Maombi yote yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani:
👉 https://portal.ajira.go.tz
xiv. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliobainishwa HAYATAFIKIRIWA.
Imetolewa na:
MKURUGENZI WA MJI
HALMASHAURI YA MJI WA BABATI
S.L.P 383,
BABATI