Kujua namba yako ya Nida Kwenye Simu yako
TANGAZO: KUJUA NAMBA YAKO YA UTAMBULISHO WA TAIFA (NIN)
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inawataarifu wananchi wote kuwa sasa wanaweza kujua Namba yao ya Utambulisho wa Taifa (NIN) kwa urahisi kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS).
Hatua za Kufata:
-
Fungua sehemu ya kutuma ujumbe (SMS) kwenye simu yako.
-
Andika ujumbe kwa mpangilio ufuatao:
-
Jina la Kwanza la Mwombaji * Jina la Mwisho la Mwombaji * Tarehe ya Kuzaliwa (Siku/Mwezi/Mwaka) * Jina la Kwanza la Mama * Jina la Mwisho la Mama
-
-
Tuma ujumbe huo kwenda namba 15274.
Mfano wa Ujumbe:
MUSA*JUMA*02031987*MARIAMALI*
Baada ya kutuma ujumbe, utapokea majibu yatakayokuonyesha Namba yako ya Utambulisho wa Taifa (NIN).
Huduma hii ni BURE.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na NIDA kupitia:
-
Tovuti: www.nida.go.tz
-
Barua pepe: info@nida.go.tz
-
Mitandao ya kijamii: @nidatzania
