Kufuatia usaili wa hatua ya kwanza kwa kada mbalimbali uliofanyika kuanzia tarehe 16 Desemba hadi 23 Desemba, 2025 katika vituo mbalimbali nchini, Tume ya Utumishi wa Mahakama (JSC) inapenda kuwataarifu waombaji wa nafasi mbalimbali ambao majina yao yameorodheshwa kwenye tangazo hili kuwa wamechaguliwa kuhudhuria usaili wa hatua ya pili (Usaili wa Ana kwa Ana – Oral Interview).
Tarehe na vituo vya usaili vimeainishwa katika orodha ya majina ya wasailiwa waliochaguliwa iliyoambatishwa na tangazo hili.
Waombaji wa kada za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II na Dereva Daraja la II wataanza na usaili wa vitendo (Practical Interview), na wale watakaofaulu ndipo watakaoendelea na usaili wa ana kwa ana (Oral Interview).
Usaili utafanyika kuanzia tarehe 5 Januari hadi 16 Januari, 2026.
Wasailiwa wote waliochaguliwa wanatakiwa kufika kwenye vituo vya usaili walivyopangiwa saa 2:00 asubuhi, wakiwa na nyaraka halisi zifuatazo:
-
Vyeti vya elimu
-
Vyeti vya taaluma
-
Cheti cha kuzaliwa
-
Kitambulisho kimojawapo kinachotambulika na Serikali chenye picha ya msailiwa, kama vile:
-
Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
-
Kitambulisho cha Mpiga Kura
-
Hati ya Kusafiria
-
Leseni ya Udereva
-
Wasailiwa watakaoshindwa kuwasilisha nyaraka zilizotajwa au watakaofika nje ya muda uliopangwa hawatasailiwa. Aidha, wasailiwa wanakumbushwa kuhudhuria usaili katika vituo walivyopangiwa pekee.
Waombaji ambao hawataona majina yao kwenye orodha wanapaswa kufahamu kuwa hawakufaulu kuingia kwenye hatua ya pili ya usaili.
Waombaji wote wanashauriwa kutembelea Tovuti ya Tume ya Utumishi wa Mahakama: www.jsc.go.tz kwa taarifa zaidi.
Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali piga simu saa 24 kupitia namba zifuatazo:
0734 219 821 au 0738 247 341,
au tuma barua pepe kupitia anuani: maulizo.ajira@jsc.go.tz