Nafasi za kazi Halmashauri ya Wilaya ya Igunga December 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi nne (04) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa mchanganuo ufuatao:-
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 04
1.1 MAJUKUMU NA KAZI
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
ii. Kupokea wageni, kuwasaidia shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine.
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
v. Kupokea majalada na kuyasambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo husika.
vi. Kukusanya, kutunza na kurekebisha majalada na nyaraka katika sehemu husika.
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.
ix. Kufanya kazi nyingine atakazoelekezwa na Msimamizi wake.
1.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI), wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha (NTA Level 6) ya Uhazili. Aidha, wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa kasi ya maneno 100 kwa dakika moja, na wawe na ujuzi wa programu za kompyuta za Ofisi kama vile Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.2 NGAZI YA MSHAHARA
TGS C
MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kubainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Curriculum Vitae – CV) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana, anuani ya barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
Provisional/Testimonials/Statement of Result na hati za matokeo ya Kidato cha Nne na Sita (Form IV na Form VI results slips) HAVITAKUBALIWA.
iv. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
v. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
vi. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya kazi kwa waajiri wao, na waajiri wajiridhishe ipasavyo.
vii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe, na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyomo kwenye Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
viii. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita (kwa waliofikia kiwango hicho) na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kulingana na sifa za kazi husika.
ix. Vyeti vya Postgraduate, Degree, Advanced Diploma, Diploma, Certificates, Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV na VI, Cheti cha Kompyuta, na Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificates kutoka Bodi husika).
x. Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA au NECTVET).
xi. Uwasilishaji wa taarifa au sifa za kughushi utachukuliwa hatua za kisheria dhidi ya wahusika.
xii. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 01 Januari, 2026.
xiv. MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga,
S.L.P. 19,
IGUNGA.
xv. Maombi yote ya kazi yatumwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) katika anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz. Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kubofya sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”.
xvi. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA