Kumbukumbu: WARAKA WA ELIMU NA. 06 WA MWAKA 2025 KUHUSU
KALENDA YA MIHULA YA MASOMO KWA SHULE ZA AWALI, MSINGI NA SEKONDARI KWA MWAKA 2026
Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.
-
Kwa kuzingatia umuhimu wa kuwa na idadi sahihi ya siku za masomo kwa mwaka kama inavyotakiwa na mitalaa, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeandaa Kalenda ya Mihula ya Masomo kwa Shule za Awali, Msingi na Sekondari (Kidato cha I–IV) kwa mwaka wa masomo 2026.
-
Ni muhimu kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Kalenda hii unafanyika kama ilivyopangwa ili kuondoa vipindi visivyo na tija katika ufundishaji na ujifunzaji, na kuhakikisha kuwa idadi ya siku za masomo zilizopangwa zinatimia. Hii itasaidia kuboresha ubora wa elimu kwa kuwawezesha wanafunzi kukamilisha mitalaa kwa wakati, pamoja na kuwawezesha walimu kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
-
Kalenda ya Mihula ya Masomo kwa Shule za Awali, Msingi na Sekondari kwa mwaka 2026 ni kama ifuatavyo:
MIHULA
| MHULA | KUANZA KWA MHULA | MAPUMZIKO YA MHULA | KUANZA TENA | KUHITIMISHA | IDADI YA SIKU ZA MASOMO |
|---|---|---|---|---|---|
| Muhula I | 06/01/2026 | 27/03/2026 | 08/04/2026 | 07/06/2026 | 97 |
| Muhula II | 16/06/2026 | 04/09/2026 | 18/09/2026 | 18/11/2026 | 102 |
Jumla ya Siku za Masomo kwa Mwaka: 199