Jinsi ya kuwasiliana na Ajira Portal UTUMISHI Namba zao za Simu
Ukitaka kuwasiliana na utumishi/ajira portal haya hapa mawasiliano yao namba zao za simu na email zao

*JINSI YA KUWASILIANA NA AJIRA PORTAL ( SECRETARIAT YA AJIRA) IKIWA UNACHANGAMOTO YA YOYOTE.*
KUNA NJIA KUU TATU ZA KUWASILIANA NAO.
- KWENDA OFISI ZA SECRETARIAT YA AJIRA DODOMA.
- KWA KUPIGA SIMU
- KWA EMAIL.
KUWASILIANA NA SECRETARIAT YA AJIRA KWA KWENDA OFISINI DODOMA MOJA KWA MOJA.
Hii ndiyo njia ya uhakika asilimia 100% kwani utakuwa na uwezo wa kueleza Tatizo lako
ENEO:Mtaa wa Mahakama Tambukareli, DODOMA
KUWASILIANA NAO KWA NJIA YA SIMU.
Njia hii ni rahisi na uhakika, lakini inahitaji uwe mvumilivu sana.
Unapo piga simu Piga Mfululizo bila kukata hata masaa mawili.
Kumbuka Wanaopiga ni wengi sana, kwahyo kuwa mvumilivu kama unashida.
Namba za Simu
1. 0262160350
2. 255739160350
*NJIA YA TATU NI KWA EMAIL.*
UNAWEZA KUWASILIANA NA AJIRA PORTAL KWA KUTUMIA EMAIL.
FANYA HIVI ILI KUWEZA KUJIBIWA HARAKA.
EMAIL ZA KUTUMIA
JINSI YA KUTUMA SHIDA YAKO.
1. Copy email bila kuzikosea na tuma kwenda email zote – utatuma kwenda katibu@ajira.go.tz na Copy kwenda malalamiko@ajira.go.tz
2. Andika Kichwa cha Shida yako Kwenye Subject section. Hakikisha email yako ina subject section.
Mfano: MAOMBI YA KUONDOA ADVANCED DIPLOMA au MAJINA KWENYE NIDA NA NECTA HAYA MATCH au NAOMBA KUFAHAMU EMAIL NA PASSWORD NILIYOTUMIA NIDA.
3. Sehemu nyingine ni COMPOSE – kwa ufupi andika maneno machache, na Majina yako, NIDA, namba za simu na email n.k
4. Hitimisho – kama una screenshot au documents yoyote unaweza ku-attach
5. Send