Jinsi ya Kuangalia Majina ya walioapa Mkopo HESL 2025/2026
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Ijumaa, Oktoba 24,2025 imetoa awamu ya kwanza ya upangaji mikopo na ruzuku yenye jumla ya wanafunzi 135,240. Idadi hii inajumuisha wanafunzi wafuatato:
i. Wanafunzi 40,952 wa shahada ya awali na wanafunzi 5,342 wa stashahada waliopangiwa mikopo kiasi cha TZS. 152 bilioni.
ii. Wanafunzi 615 wa Samia Skolashipu waliopangiwa ruzuku kiasi cha TZS. 3.3 bilioni.
iii. Wanafunzi 88,331 wanaoendelea na masomo wamepangiwa mkopo kiasi cha TZS. 271.2 bilioni baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka uliotangulia.
Bodi ya Mikopo itaendelea kutoa awamu zingine za mikopo na skolashipu kadiri itakavyopokea uthibitisho wa udahili kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na matokeo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo.
Aidha, Bodi ya Mikopo inawakumbusha waombaji wa mikopo na ruzuku kuendelea kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia ‘SIPA’ wakati taratibu za uchambuzi na upangaji wa mikopo na ruzuku zikiendelea.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
Ijumaa, Oktoba 24, 2025
| Hatua | Maelezo ya Kufanya |
|---|---|
| 1. Fungua Tovuti Rasmi ya HESLB | Nenda kwenye tovuti ya https://olas.heslb.go.tz kupitia simu au kompyuta yenye intaneti. |
| 2. Bonyeza “Login to OLAMS” | Ukifika kwenye ukurasa wa mwanzo, chagua sehemu ya “Login to OLAMS” au “SIPA Account” kwa waombaji wa mkopo. |
| 3. Ingiza Taarifa Zako za Kuingia | Andika Email au Namba ya Maombi (Form Four Index Number) pamoja na Neno la Siri (Password) ulilounda wakati wa kujisajili. |
| 4. Fungua Dashibodi Yako | Baada ya kuingia, utaona dashibodi yako ya OLAMS yenye taarifa zako binafsi na za mkopo. |
| 5. Bonyeza Sehemu ya “Loan Status” | Chagua kipengele cha “Loan Status” au “Allocation Results” ili kuona kama umepewa mkopo na kiasi kilichotolewa. |
| 6. Pakua au Chapisha Taarifa | Unaweza kupakua (Download) au kuchapisha (Print) taarifa ya mkopo kwa matumizi yako ya baadaye. |
| 7. Kagua Mara kwa Mara | Ikiwa majibu yako hayajatoka, endelea kuangalia mara kwa mara kwani HESLB huendelea kusasisha orodha kwa awamu tofauti. |