Posho za walimu wa kujitolea 2025
Serikali imetangaza kuwa walimu watapewa fursa ya kufanya kazi za kujitolea mashuleni kwa makubaliano maalumu na malipo maalumu
Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Deus Sangu, aliliambia Bunge Ijumaa Mei 2, 2025, kuwa mwongozo huo utaanza kutumika rasmi kuanzia Julai Mosi, 2025.
Naibu Waziri alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Arumeru Magharibi, Noah Saputu, ambaye aliuliza ni lini Serikali itakamilisha mwongozo wa kutoa kipaumbele katika ajira zinazotangazwa kwa wanaojitolea.
Katika swali la nyongeza, Mbunge huyo alihoji ni kwa nini Serikali isitangaze mpango huo sambamba na malipo kwa vijana wanaojitolea.
Katika malipo hayo serikali imesema waalimu hao watalipwa kama ifuatavyo:
- Walimu wa kujitolea shule za msingi watalipwa kiasi cha kuanzia Tsh 250,000/=
- Walimu wa kujitolea kwa shule za sekondari wao watalipwa kiasi cha kuanzia Tsh 300,000/=
Malipo hayo yote yatatokana na bajeti ya mapato ya ndani ya Halmashauri husika.
Very good partnership https://shorturl.fm/9fnIC
https://shorturl.fm/FIJkD
Naomba ajira