Taarifa Kutoka JWTZ Kwa Waombaji wote wa Ajira za JWTZ 2025
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) April 30, 2025 lilitangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye Elimu kuanzia ya Sekondari hadi Elimu ya Juu.
Katika moja ya sifa ya Kuandikishwa Jeshini mwaka huu wa 2025 ilikuwepo ya Kijana awe amehitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mkataba wa kujitolea au Mujibu wa Sheria na kutunukiwa cheti.
Kutokana na Sifa hiyo imeonekana Vijana ambao hawakupita JKT na wana sifa zingine ni wengi hivo Kanali Gaudentius Gervas Ilonda ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) ametoa Ufafanuzi Kuhusu Vijana hao Waliopita JKT na ambao hawajapita JKT Kuandikishwa Jeshini 2025.
JWTZ wamefanya hivyo baada ya mjadala mkubwa kuibuka Bungeni kuhusu kigezo hicho cha JKT kwa sababu mwanzoni bunge liliazimia kigezo hicho kufutwa kwenye ajira za vyombo vya ulinzi na usalama.
Others did not get an ID card ,they have only NIDA number how about this ?,,,because inorder to qualify as applicant supposed to make a copy of NIDA card on the attachment,,,so they are not required to make an application too !?
Waseme tuu JKT haipo maana kama wanakua wanasumbua watu na vijana wanaopitia JKT wanakua wanaonekana hawana thamani kwahiyo bora waseme tuu JKT haipo tujue moja