Mfahamu Papa Mpya LEO XIV
Leo ni siku ya furaha zaidi kwa wakatoliki duniani kwote mara baada ya kumpata Papa Mpya atakayerithi kiti ya Papa Francis uchaguzi huo ulioanza jana May 7 na kuhitimishwa May 8 mara baada ya Moshi mweupe kuonekana kwenye bomba la juu la Kanisa la Sistine ikimaanisha kuwa Papa mpya amepatikana.
Mmarekani Roberto Francis amechaguliwa kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliki akiwa amehudumu Kama Kadinali wa Chicago
Atatambulika Kama Papa LEO XIV
Hebamus Papam yani Papa tunaye. Ni Robert Francis Prevost, aliyekua kiongozi wa Dikasteri ya Maaskofu na Rais wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini tangu mwaka 2023. Kabla ya hapo alihudumu kama Askofu wa Chiclayo nchini Peru kutoka 2015 hadi 2023. Kabla ya kuwa Askofu wa Chiclayo alikuwa mkuu wa shirika la Mtakatifu Agustino (OSA) kutoka mwaka 2001 hadi 2013.
Amezaliwa mwaka 1955 huko Chicago, Illinois nchini Marekani. Ni msomi mwenye degree 5. Alipata daraja takatifu la Upadri mwaka 1982 baada ya kuhitimu shahada ya Falsafa (Bachelor degree in Philosphy) na Shahada ya Theolojia (Bachelor degree in theology) huko Illinois, Calfornia. Mwaka 1984 alitumwa masomoni nchini Italia na kuhitimu shahada ya kwanza ya sheria za Kanisa katika Chuo kikuu cha Mtakatifu Thomas wa Aquinos kilichopo Rome.
Mwaka 1987 alihitimu Shahada ya umahiri katika sheria za Kanisa (Juris Canonici Licentiatus) na baadae Shahada ya uzamivu katika sheria za Kanisa (Juris Canonici Doctor) kutoka Pontifical College of St. Thomas Aquinas.
Kisha alirudi Marekani na kutumwa umisheni huko Amerika ya kusini ambapo alitumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Askofu wa jimbo la Chiclayo nchini Peru. Mwaka 2015 aliomba na kupewa uraia wa Peru. Leo Mei 8, 2025, amechaguliwa kuwa Papa wa 267 akimridhi Papa Francis, na amechagua kutumia jina Leo XIV.
Papa Leo XIV anakua Papa wa kwanza kutoka Marekani. Pia ndiye Papa wa kwanza kuongea kwa lugha nyingi zaidi. Anaongea lugha 6 ambazo ni Kingereza, Kispaniola, Kilatini, Kifaransa, Kireno na Kijerumani. Hebamus Papam, ni neno la Kilatini linalomaanisha Papa tunaye. Vijana wa “Buza” msije kumalizia kwa kusema “Tunatamba nae”