Majina ya waliopata Mkopo Diploma 2025 HESLB
MIKOPO YA WANAFUNZI WA STASHAHADA KWA WANUFAIKA WALIOOMBA KWENYE DIRISHA LA MWEZI MACHI 2025
Wanafunzi 873 wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 1.9 Bilioni
Tunawatangazia wanafunzi wote walioomba mikopo kwa ajili ya dirisha la mwezi Machi, kwamba jumla ya waombaji 873 wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 1,944,922,500.00.
Katika awamu hii, mikopo imepangwa kama ifuatavyo:
– Chakula na Malazi (MA) yenye thamani ya TZS 1,519,788,750.00
– Ada ya Mafunzo (TU) yenye thamani ya TZS 408,433,750.00 na
– Vitabu na viandikwa (BS) yenye thamani ya TZS 16,700,000.00.
Kwa taarifa hii, wanafunzi walioomba mikopo wanashauriwa kuangalia taarifa zao kupitia akaunti walizoombea mikopo (SIPA). Wanafunzi husika pia watatakiwa kujisajili katika mfumo wa malipo wa kidigitali (DiDis) kupitia Maafisa Mikopo wa vyuo vyao.
Itakumbukwa kuwa Dirisha la mwezi Machi lilifunguliwa tarehe 15 Januari 2025 hadi 15 Februari 2025.
Hadi kufikia tarehe 02 Mei, 2025, jumla ya wanafunzi 8,438 wa stashahada wamenufaika na mikopo yenye thamani ya TZS 22,072,267,601.00 kwa mwaka 2024/2025.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji