Majibu Ya CAS Kwa Mechi ya Simba na Yanga 2025
Yanga wameshindwa kwenye kesi yao ya awali waliyofungua kwenye mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS)
Yanga katika kesi hiyo ya msingi waliyoifungua dhidi ya TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC wameomba kupewa alama 3 na mabao 3, lakini ikaiomba CAS pia izuie tarehe ya ‘DABİ’ isipangwe mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa, yani ile ya kudai alama 3 na mabao 3 kwa walichosema kua Simba SC waligomea mchezo wa tarehe 8 Machi,2025.
Walalamikiwa Simba SC, TFF na Bodi ya Ligi kwenye utetezi wao walipinga Yanga kufungua kesi CAS na kuzivuka mamlaka za TFF za kisheria.
Kwenye hukumu CAS wamekubaliana na Simba SC, TFF na Bodi ya Ligi kwamba wao CAS hawana mamlaka ya kuzuia kupangwa kwa tarehe ya DABI, lakini pia wamekubaliana na walalamikiwa kwamba wao CAS hawana haki pia ya kushughulikia jambo hili kabla halijapitia kwenye mamlaka za kisheria za TFF.
Hivyo basi shauri la Yanga SC limepigwa chini na sasa TFF na BODI YA LİGİ wako huru kupanga tarehe ya DABI na itapigwa kama kawaida.
Kwa hukumu hii Yanga wakigomea kucheza DABI itakapopangwa, maana yake ni kwamba watapokonywa alama 15, wako tayari kwa hilo? Msimamo wao ulikuwa hakuna kucheza hiyo mechi lakini walikuwa wanategemea CAS ambako wamepigwa za uso tena pamoja na lundo na mawakili walio orodheshwa huko CAS. Dabi haina kipengele, kipengele uje nacho wewe.