Sifa na Vigezo vya Kujiunga na JWTZ 2025
Mkuu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jenerali Jocob John Mkunda ametangaza nafasi za kuandikishwa Jeshi la wananchi Kwa vijana wenye elimu ya Sekondari hadi elimu ya Juu.
Akizungumza leo aprili 30,2025 Makao ya Jeshi Hilo msalato Jijini Dodoma Kwa Niaba ya Mkuu huyo wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania Msemaji wa Jeshi hilo Kanali Gaudentius Ilonda amesema kuwa nafasi zinazoandikishwa na Jeshi hilo ni kwa vijana wenye elimu ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umri usiozidi miaka 24, Vijana wenye elimu ya Stashahada umri usiozidi miaka 26, Vijana wenye elimu ya Juu umri usiozidi miaka 27 na Madaktari Bingwa wa Binadamu umri usiozidi miaka 35 ya kuzaliwa.
Uandikishaji
- Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo: –
- Awe raia wa Tanzania
- Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..
- Awe hajaoa/hajaolewa
- Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
- Awe na tabia na mwenendo mzuri
- Awe na akili timamu na afya nzuri
Masharti ya Utumishi
- Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.
- Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.
Maafisa
Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board)
huwafanyia usaili Askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za Askari wapya (Recruitment Schools).
Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya Uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.
BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI
SOMA HII
I accept it.