Jinsi Mazishi ya Papa Yanavyofanyika
Mazishi ya Papa kwa kawaida huwa ni hafla kubwa ya heshima ya juu, lakini hivi karibuni Papa Francis aliidhinisha mipango ya kufanya utaratibu mzima wa mazishi yake endapo akifariki uwe rahisi zaidi.
Mapapa waliotangulia walizikwa ndani ya majeneza matatu yaliyopangwa kwa kufuatana: la mti wa cypress, la risasi (lead), na la mwaloni (oak).
Lakini Papa Francis amechagua kuzikwa katika jeneza rahisi la mbao lililowekwa ndani ya bati la zinki.
Aidha, ameondoa utamaduni wa kuweka mwili wa Papa juu ya jukwaa maalumu linaloitwa catafalque – ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya watu kuuaga hadharani.
Badala yake, waombolezaji wataalikwa kutoa heshima zao wakati mwili wake ukiwa ndani ya jeneza lenye mfuniko ulioondolewa.
Francis pia atakuwa Papa wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya karne moja kuzikwa nje ya Vatican.
Atazikwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Major (Basilica of St Mary Major), mojawapo ya makanisa makuu manne ya kipapa jijini Roma.
PAPA FRANCIS AMEFARIKI LEO APRIL 21 2025 NYUMBANI KWAKE VATCAN
Chanzo: BBC