Majina ya walioitwa kazini Benki Kuuu Tanzania BOT 2025
Naibu Gavana Utawala na Udhibiti wa Ndani wa Benki Kuu ya Tanzania anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote waliofanya usaili wa mahojiano tarehe 21, 24 na 25 Machi, 2025 kuwa majina ya waombaji kazi waliofaulu
usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Aidha ajira zao zitakuwa rasmi pale vyeti vyao vitakapohakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika.
Waombaji waliofaulu usaili watatakiwa kufika Benki Kuu ya Tanzania Makao Makuu Ndogo Dar es Salaam tarehe 23 Aprili, 2025 Saa Mbili na Nusu Asubuhi ili kukamilisha taratibu mbalimbali za Ajira, wakiwa na nyaraka zilizoainishwa katika tangazo hili kwa uhakiki.