Majina ya walioitwa kwenye usaili TARURA Manyara 2025
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala za Serikali Sura Na. 245 na kutangazwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali Na. 211 la tarehe 12 Mei 2017. Wakala ulianza kufanya kazi rasmi tarehe 1 Julai 2017 na sasa Wakala umefikisha takribani miaka 5 toka kuanzishwa kwake.Lengo Kuu la Uanzishwaji wa TARURAni kukabiliana na changamoto zilizojitokeza wakati jukumu la Menejimenti ya Mtandao wa Barabara za Wilaya lilipokuwachini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa(MSM) 184, lakini vilevile pamoja na kukabiliana na mabadiliko katika sekta ya barabara kwa nia ya kuboresha huduma na kuongeza ufanisi.Jukumu kubwa la TARURA ni kusimamia matengenezo, ukarabati na ujenzi wa Mtandao wa Barabara za Wilaya wenye jumla ya Kilomita 144,429.77 zilizokuwa zikisimamiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa 184 na kuratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI chini ya Idara ya Miundombinu.
YAFUATAYO NI MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI TARURA MKOA WA MANYARA