Tangazo la Nafasi 8,000 za Mafunzo ya Ufundi Stadi katika Fani Mbalimbali 2025
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu inatekelezaProgramu ya Kukuza Ujuzi Nchini inayolenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifakupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira.Ofisi imeingia makubaliano na vyuo 52 vinavyotoa mafunzo ya ufundi stadiambavyo vimesajiliwa na Mamlaka husika kutoa mafunzo katika fani mbalimbalizikijumuisha ubunifu wa Mitindo na Ushonaji Nguo, Ufundi Bomba, Uashi,Useremala, Uchomeleaji na uungaji vyuma, Upakaji rangi na maandishi yaalama, Upishi, Utengenezaji wa vipuri vya mitambo, Ufundi Magari naMitambo, umeme wa majumbani na viwandani, Umeme wa Magari, Hudumaza Hoteli na Utalii, Ukataji Madini na Ufundi vyuma.